Nchini Kenya, Gen Z (vijana wa kati ya umri wa miaka 17-28) wamekuwa wakiendesha kampeni mitandaoni hadi mitaani ili kuiwajibisha serikali. Lakini swali linaloibuka ni je, baadhi yao wanatumika kisiasa? Na ni mbinu gani bora zaidi wanayoweza kuitumia kufuatia hali ya sasa ya kisiasa? Wakio Mbogho amelijadili suala hilo pamoja na vijana nchini Kenya kwenye kipindi cha Vijana Tugutuke.