Jean-Claude ataka kukomeshwa kwa ukaguzi wa mipaka katika EU
23 Novemba 2024Matangazo
Kiongozi huyo wa zamani ameliambia shirika la utangazaji la hapa Ujerumani DPA kwamba yeyote anaefikiri anaweza kuwakamata wakimbizi na watu wengine kwa waranti ni kosa. Alisema kuwa wasafirishaji haramu wanafanya kila wawezalo kuepuka ukaguzi rasmi wa polisi. Na kuongezaa kwamba ukweli huo unajidhihirisha katika maeneo ya Luxembourg, ambao kuna kuwa na msongamano mkubwa juu ya mipaka ya Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji. Ujerumani ilirejesha hatua za ukaguzi wa mipaka yake yote Septemba 16, kwa lengo la kudhibiti wimbi la wahamiaji na kulinda usalama wa ndani. Hatua ambayo pia inatekelezwa na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.