Jeshi la Congo na MONUSCO watangaza operesheni ya pamoja
4 Novemba 2023Matangazo
Tangazo hilo linafuatia kuongezeka kwa makabiliano na kundi la M23 tangu mwezi uliopita, ambayo yamewalazimu watu 200,000 kuyakimbia makazi yao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, baada ya kushuhudiwa kipindi cha utulivu.
Hili pia limejiri baada ya serikali ya Congo kuomba jeshi hilo liondoke. Akiwahutubia waandishi habari katika mji wa mashariki wa Goma, Kamanda Mkuu wa Jeshi la MONUSCO Otavio Rodrigues de Miranda Filho alisema kuongezeka kwa machafuko katika siku za karibuni kunatia wasiwasi.
Alifafanua kuwa operesheni mpya ya kijeshi ya pamoja na jeshi la Congo, ilinayoitwa Springbok italenga kulinda mji wa Goma na mji ulio karibu wa Sake. Miranda Filho amesema M23 sasa inasonga mbele kuelekea Sake.