Jopo la WHO lasema mpox bado ni kitisho cha afya duniani
23 Novemba 2024Matangazo
Ulijiri miezi mitatu baada ya WHO mwezi Agosti kutangaza dharura ya afya kutokana na kusambaa kwa mpox, ikifahamika awali kama homa ya nyani, barani Afrika.
Soma pia:Kongo yakabiliwa na uhaba wa chanjo ya Mpox
Aina mpya ya kirusi cha ugonjwa huo, inayofahamika kama Clade 1b, ambacho kilisambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazusha hofu ya kusababisha magonjwa mengine makali zaidi.
Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya visa 50,000 vinavyoshukiwa kuwa vya mpox viliripotiwa kwenye nchi za Kiafrika mwaka huu. Kulikuwa na zaidi ya vifo vya watu 1,080. Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya kinakadiria hatari ya mpox kwa umma barani Ulaya kuwa ndogo.