Kansela Schröder hatang'atuka
25 Septemba 2005Berlin:
Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amesema leo kuwa anashikilia msimamo wake wa kuendelea kushika wadhifa huo ingawaje kuna shinikizo la kumtaka ang’atuke baada ya uchaguzi mkuu uliofanywa juma lililopita kutompata mshindi. Ameiambia Idhaa ya Kwanza ya Televisheni ya Ujerumani ARD kuwa hana sababu hata kidogo ya kubadilisha msimamo wake eti kwa sababu anashinikizwa na baadhi ya vyombo vya habari na vyama vya upinzani. Amesema kuwa suala la nani aiongoze Ujerumani litatatuliwa wakati wa mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto. Kansela Schröder na mgombea wa kihafidhina, Bibi Angela Merkel wanadai wadhifa huo. Chama tawala cha SPD kitakutana na vyama ndugu vya upinzani vya Christian Democratic (CDU) Christian Social (CSU) Jumatano ijayo na kuendelea na mazungumzo yao ya muungano.