Kenya kuviondoa vikosi vya jeshi Somalia
5 Machi 2020Matangazo
Hatua hiyo inatarajiwa kuchukuliwa baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa tamko la onyo kali saa chache zilizopita dhidi ya Somalia kuhusu kile alichokiita uingiliaji wa mamlaka ya maeneo ya nchi yake.
Hatua hiyo itakuwa ni kukifikisha mwisho kipindi cha takribani miaka minane ya uvamizi uliofanywa na jeshi la Kenya KDF kwa lengo la kukabiliana na kundi la al-shabaab nchini Somalia.
Katika kile kinacholezwa kutokea Jumatatu iliyopita, serikali ya Kenya imesema jeshi la Somalia lilivuka mpaka na kuharibu mali za Wakenya katika mji wa Mandera, ambao upo mpakani na Somalia.
Hata hivyo waziri wa habari wa Somalia hakuweza kupatikana mara moja kujibu malalamiko ya Kenya.