JamiiSudan
Kiongozi wa NRC aonya Ulaya kuhusu kuipuuza Sudan
24 Novemba 2024Matangazo
Mkuu wa Baraza la wakimbizi la Norway, NRC, amesema mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan ni mbaya zaidi kuliko migogoro ya Ukraine, Gaza na Somalia kwa pamoja. Kwenye mahojiano na shirika la habari la Ujerumani DPA, Jan Egeland amesema maisha ya watu milioni 24 yako hatarini nchini Sudan. Egeland aliyefanya ziara Darfur Magharibi na maeneo mengine ya Sudan, amehuzunishwa kuona ulimwengu umeifumbia macho idadi inayoongezeka ya watu wanaokumbwa na njaa nchini humo. Amesema ikiwa sote tunakubali kwamba maisha ya mwanadamu ni ya thamani sawa, basi Sudan inapaswa kupewa kipaumbele.
Mkuu huyo wa shirika la NRC alishuhudia nyumba zilizoharibiwa na vitongoji vilivyochomwa kufuatia mzozo huo wa Sudan, ambao unaendelea kwa takriban siku mia sita.